Tukio hilo limejiri asubuhi ya saa 12 alfajiri ambapo gari hilo lilikuwa likipita kwa kasi bila kufuata alama za barabarani zinazoonesha sehemu ya reli.
Akizungumza na mwandishi wetu, Ofisa Oparesheni Shirika la Reli, Mohamed Kanka, alisema kuwa treni hiyo ilikuwa ikipita majira ya saa kumi na mbili alfajiri na kugongwa na gari iliyokuwa ikipita pasipo dereva wa gari hiyo kuzingatia alama iliyokuwa ikionesha kama sehemu hiyo kuna reli.
Alisema kuwa katika ajali hiyo dereva wa gari na dereva aliyekuwa katika treni hiyo wameumia na wamekimbizwa Hospitali ya Amana Ilala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Vilevile alisema baada ya ajali hiyo kutokea gari jingine lililokuwa limesimama liligongwa na kichwa cha treni baada ya kuiacha njia yake na kuelekea upande wa magari yaliyokuwa yakipita.
Ofisa huyo amewaasa madereva kuwa makini wanapofika eneo lenye alama kuonyesha mbele kuna reli kwani ajali nyingi hutokea kutokana na madereva wasiokuwa waangalifu. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment