"Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine".
Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.
Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.
Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.
Imetolewa na:
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment