President wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea na kumjulia hali makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kwenye
hoteli ya Serena Dar es salaam ambako anapata mapumziko baada ya
kuruhusiwa kutoka hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelazwa kwa
matibabu.
Pamoja na kumpa mkono wa pole, Rais Magufuli amemuombea Maalim Seif Shariff Hamad kupona haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida na kuyasema haya >>> ‘Nilishtushwa
sana na taarifa za kuugua kwako lakini sasa nafurahi kukuona ukiwa
mwenye afya nzuri ikilinganishwa na taarifa nilizozipata hapo awali,
nakupa pole sana”
Kwenye
taarifa iliyotumwa na Ikulu kwa millardayo.com , Maalim Seif Shariff
Hamad amemshukuru Rais Magufuli kwa ukarimu na upendo aliouonesha kwa
kumtembelea hotelini hapo na amewahakikishia watanzania kuwa hali yake
sasa inakwenda vizuri na inazidi kuimarika kila kukicha.
“Sasa
hivi ninaweza kutembea vizuri, kufanya shughuli zote mwenyewe bila ya
msaada wa mtu yeyote yule, na ni matumaini yangu kwamba baada ya muda
mfupi, hali yangu itarudi kama kawaida, nije nishirikiane na watanzania
wenzangu katika kutekeleza majukumu ya nchi yetu“ Maalim Seif alimweleza Rais Magufuli.
Maalim Seif alipatwa na kizunguzungu kikali akiwa uwanja wa ndege Zanzibar akielekea Dar es salaam juzi ambapo ilibidi aombe msaada wa watu kumsaidia kupanda ndege, alipofika Dar na kulazwa Hospitali uchunguzi ulionyesha hakuwa na tatizo lolote bali ni uchovu tu.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment