‘Akibananishwa ukutani’ na mwandishi wetu kwa maswali magumu hivi karibuni, Aunt alisema amekuwa akiumizwa na maneno yanayoendelea juu ya kumzidi umri Iyobo, na kusema hayuko tayari kuona uhusiano huo ukivunjwa kwa maneno ya aliowaita “wakosa kazi”.
“Kwani wakati tunatongozana hatukujua kuwa tunazidiana umri? Mbona watu wanashindwa kufanya mambo ya msingi na kukalia majungu? Kwetu sisi suala la umri ni namba tu, labda nikuulize, ulishaona mtoto anambebesha mwanamke mimba? Maneno ya mimi kumzidi umri Iyobo yananiumiza sana kwa kweli, lakini nitaulinda uhusiano huu hadi mwisho,” alisema Aunt Ezekiel
Chanzo: GPL WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment