Akizungumza katika Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana, Nape alisema kuna taarifa za uhakika kuwa kuna baadhi ya makundi ya Ukawa yamepanga mchezo huo wa kutengeza kadi bandia.
“Wameanza kuratibu mchezo huo ili wazigawe kadi hizo kwa watu wao, ili baadaye asipopita mgombea wao, ionekane wana CCM wanakihama chama chao kwa kurudisha kadi hizo kwenye shughuli mbalimbali za vyama hivyo vinavyounda Ukawa.
“Wakati tunachunguza kwa kina suala hilo, Ukawa waache mchezo huo wa ovyo na Watanzania wakwepe mchezo huo na wawe makini,” alisema WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment