Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » , » Kanisa Lagoma Kumbatiza Mtoto wa Aunt Ezekiel

Kanisa Lagoma Kumbatiza Mtoto wa Aunt Ezekiel

Kanisa Katoliki limemzuia staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel kumbatiza mwanaye kutokana na kutokidhi matakwa ya kanisa.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni mara baada ya mwigizaji huyo ambaye imani yake ni ya Kiislamu, kutaka kumbatiza mwanaye huyo ambaye baba yake ( Moze Iyobo) ni Mkatoliki.

“Alikuwa amejipanga kumbatiza Kikristo kutokana na imani ya baba mtoto wake lakini alipokutana na padri Paul Ruwaaich wa Parokia ya Uparo Moshi aliyekuwa Dar kikazi akamtaka akaanzie kusali kwenye Jumuiya Ndogondogo (mtaani kwake), abadilishe dini ndipo mtoto huyo abatizwe kwani ndizo taratibu za Kanisa Katoliki.

“Alipopewa sharti hilo, lilikuwa gumu kwa Aunt, ikabisi ageuze zake,” kilisema chanzo chetu.

Mwanahabari wetu alipomuuliza Aunt kuhusu suala hilo, alisema amebaki njia panda na anatafakari cha kufanya. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips