DR Slaa Kuibukia CCM, Apangwa Kujitokeza Kwenye Mkutano wa CCM Jagwani.....
USHAWISHI mkubwa umefanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha kuwa, katibu mkuu aliye mapumzikoni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wallboard Slaa anashiriki kwenye kampeni ya chama hicho tawala, Uwazi Mizengwe limeambiwa. Chanzo kutoka ndani ya CCM kilisema hivi karibuni kuwa, mazungumzo yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa na kwamba upo uwezekano wa asilimia 90 kwa Dk. Slaa kupanda jukwaani siku ya ufunguzi wa kampeni za CCM uliopangwa kufanyika kwenye Viwanja vya Jangwani, Dar kesho Jumapili. “Ili kukabili nguvu ya upinzani tulipanga kuwa Dokta atoke mafichoni ashiriki nasi kwenye uzinduzi, tuna imani hilo litafanikiwa na utakuwa ni mtaji mkubwa kwa chama chetu kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu,” kilisema chanzo chetu. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja
Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog
0 comments:
Post a Comment