Mbali na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira uwanjani, Didier Drogba
raia wa Ivory Coast amekuwa na mchango mkubwa katika shughuli za
kijamii ambazo ambazo amekuwa akishiriki ndani ya nchi yake na Afrika
pia.
Uongozi wa ligi kuu ya England FA
umeridhishwa na kazi yake.. wameamua kumpa tuzo kutokana na mchango
wake mkubwa wa kuhamasisha soka la vijana Afrika na uamuzi wake wa
kufungua Didier Drogba Foundation ambayo itakuwa ikifanya kazi ya kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali.
Staa huyo wa soka wa Chelsea amepewa heshima hiyo kama sehemu ya kumpongeza kwa kazi nzuri za kijamii anazofanya.
Tayari Drogba amejenga hospitali kubwa ya kisasa nchini kwao Ivory Coast.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment