Ishu ya Gwajima ni kama ndio imeanza upya baada ya kutakiwa kuleta
nyaraka kumi muhimu, zikiwemo returns za hesabu zake za kanisa, bodi ya
wadhamini, hati ya usajili wa kanisa, namba ya utambulisho, jumla ya
makanisa yake, mali anazimiliki nk
Kwa juu juu ni rahisi kuona hili ni jambo jepesi lakini kiuhalisia huu
unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa enzi za gwajima. Kila nyaraka
atakayoleta itachambuliwa kwa vigezo vyote na kwakweli nyingi ya nyaraka
hizo (kama zitakuwepo) zitakuwa na mushkeli
Na mushkeli utakaotokea kwenye kila nyaraka utaangaliwa kwa jicho la
kisheria na adhabu zake, hii ni msiba kwa yoyote yule ambaye anafanyiwa
ukaguzi na serikali, yataibuka mengi mengi ambayo hayajulikani, kuanzia
mamlaka ya mapato, vyeti na usajili, uhamiaji, taratibu za kuendesha
kanisa nk nk
Pamoja na kashfa zake nyingi lakini hii ishu ni ya kisiasa zaidi, na hii
inatokana kuweka wazi msimamo wake bila woga wa kuwaunga mkono watu
wawili muhimu kwenye uchaguzi mkuu ujao Lowassa na Dr Slaa, hawa wawili
hawa ni homa mbaya kwa ccm kwasasa, yeyote atakayefanikiwa kuchukua
madaraka ni kiama kwa ccm, japo El yupo ccm
Gwajima anaponzwa na kujiamini kulikopitiliza na kuchanganya na siasa za
makundi, hawatamuacha hadi wahakikishe wamemmaliza kabisa
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment