Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mastaa wa soka na wapenzi wao.. Hawa kumi wametajwa kuvutia watu wengi zaidi

Mastaa wa soka na wapenzi wao.. Hawa kumi wametajwa kuvutia watu wengi zaidi

Couples-76 
Soka ndio mchezo wenye mashabiki wengi zaidi duniani, lakini watu huvutiwa na mastaa wa soka na wengine hufuatilia hata maisha yao nje ya soka yakoje, ndio maana mtu kama Beckham na familia yake wamekuwa wakifuatiliwa sana maisha yao licha ya kustaafu soka.
Hapa nimekuwekea list ya mastaa ambao hutazamwa zaidi na watu wengi katika maisha yao ya mahusiano ya kimapenzi.

1. David na Victoria Beckham
bee
Unaambiwa hii ndiyo couple  iliyokuwa na nguvu zaidi kwa upande wa wanasoka baada ya kufunga ndoa rasmi mwaka 1997, Beckham na mke wake Victoria wana watoto wanne ambao ni Brooklyn, Harper, Romeo na Cruz

2. Lionel Messi na Antonella Roccuzzo
mee
Messi na mke wake ambao wote ni raia wa Argentina walianza mahusiano yao rasmi mwaka 2009, kwa sasa wana mtoto mmoja aitwaye Thiago aliyezaliwa Novemba 2012

3. Steven na Alex Gerrard
gee
Hii pia ni miongoni mwa couple yenye nguvu kubwa katika soka la England na imekuwa ikitazamwa na watu wengi, wana watoto watatu Lilly, Lourdes na Lexie

4. Gerard Pique na Shakira
shak
Camera za mapaparazzi zilikuwa karibu nao tangu walipoanza uhusiano wakati Shakira alipopata shavu la kufanya video ya wimbo wa ‘Waka Waka’ uliotumika wakati wa kombe la dunia mwaka 2010, wana watoto wawili, Sasha na Milan

5. Frank Lampard na Christine Bleakley
lamp
Walikutana wakati ambao Lampard alipoachana na mchumba wake ambaye wamezaa mtoto mmoja Elen, waliingia rasmi kwenye uhusiano mwaka 2011

 6. Wesley Sneijder na Yolanthe
snei
Sneijder na mkewe ambao ni raia wa Uholanzi walianza uhusiano mwaka 2009 na mwaka uliofuata waliamua kufunga ndoa

7. Iker Casillas na Sara Carbonero
iker
Walianza uhusiano wao mwaka 2009, mpaka sasa wana mtoto mmoja anayeitwa Martin aliyezaliwa January 2010

8. Wyne Bridge na Frankie Sandford
briii
Uhusiano wao ulianza mwaka 2010 wakati Bridge akiwa Manchester City, walifunga ndoa mwaka 2014 na sasa wana mtoto mmoja anaitwa Parker

9. Peter Crouch na Abbey Clancy
croo
Crouch na Clancy wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu tangu mwaka 2006, wamejaliwa mtoto mmoja wa kike ambaye jina lake ni Sophia

10. Gareth Bale na Emma Rhys 
bale
Uhusiano wao huenda ukawa kwenye rekodi kubwa zaidi, walianza urafiki tangu wakiwa wadogo sana, safari ikafika hapa ukubwani sasa.. ni mume na mke, wana mtoto mmoja ambaye anaitwa Alba Violet
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips