Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Shilole: Ninapenda Kugombea Ubunge Igunga lakini Nahofia Maisha Yangu

Shilole: Ninapenda Kugombea Ubunge Igunga lakini Nahofia Maisha Yangu

Shilole bado ana nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Igunga, lakini anahofia kuwa maisha yake yanaweza kuwa hatarini!

Shilole ameiambia Bongo5 kuwa amepokea simu nyingi kutoka Igunga zinazomtaka ajitose kuwania nafasi hiyo, lakini bado yupo njia panda.

Unajua siasa ni ngumu mimi bado nipo kwenye mjadala wa kugombea na hii ni baada ya kuona watu wanataka kuongozwa, lakini bado nafikiria,” amesema. “Nikiwa tayari nitagombea kupitia CCM. Kitu ambacho kinaniogopesha kiukweli ukiangaliwa watu waliopita ni vijana tu wanakufa mapema kutokana na mambo ya siasa. Siasa inahitaji moyo sana mimi ni muoga sana, naogopa kufa watu wanauwana! Mtu unatamani lakini ndo hivyo,” ameongeza.

Mimi napigiwa simu nyumbani Igunga, watu wengi sana kila mmoja ananiambia ‘tunakuhitaji ugombe yaani baada ya Rostam wananihitaji mimi! Mimi bado nipo njia panda mpaka sasa hivi lakini muda ukifika kila kitu mtasikia.” WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips