Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mtoto wa Mwisho wa Rais Kikwete Ataka Ubunge B’moyo, Atamba ana Uwezo wa Kuongoza

Mtoto wa Mwisho wa Rais Kikwete Ataka Ubunge B’moyo, Atamba ana Uwezo wa Kuongoza

Makada wawili wa CCM wilayani Bagamoyo,  wameonyesha nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo hilo kupambana na mbunge wa sasa, Dk Shukuru Kawambwa.

Makada hao ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Dunda, Yusufu Mrisho Kikwete ambaye ni kitinda mimba wa familia ya Rais Jakaya Kikwete na Abdursharrif Zahoro ambaye  ni mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi  CCM wilayani humo.

Wakati  makada hao wakitangaza nia hiyo  juzi, tayari  mbunge wa jimbo hilo Dk Shukuru Kawambwa  alikwisha tangaza nia ya kutaka kutetea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Naye Yusuph Kikwete alisema  ana matumaini makubwa ya kushinda kwa kuwa, amekuwa akiungwa mkono na makundi mbalimbali, wakiwamo vijana ambao wamekuwa wakimshawishi kugombea nafasi hiyo.

 “Ni kweli kuna makundi mengi, yamekuwa yakinishawishi kuingia katika kinyang’anyiro na baada ya kutafakari sana na kujipima kama ilivyo kwa wanasiasa wengine, nimeona siwezi kukataa ushawishi huo, maana kuna watu wameona uwezo wangu  wa kiuongozi,” alisema. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips