TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na familia ya staa huyo, ndugu wa karibu akiwemo mama, binamu yake Romy Jons, wajomba zake, mameneja na marafiki wa karibu wa familia, waliamua kuweka kikao hicho usiku hivi karibuni ili Diamond athibitishe kama kweli kiumbe kinachoripotiwa kuwa ni cha kwake magazetini ni chake kweli.
“Ndugu walichachamaa, walitaka kujua kama kweli mimba inamhusu Diamond au ni magumashi ya kiki za vyombo vya habari.
“Kwenye hicho kikao walimualika na Diamond mwenyewe ili aweze kufunguka kama ana uhakika kweli mimba ni yake,” kilisema chanzo hicho
WALITAKA ATOE MSIMAMO
“Mbali na kutaka kujua kama mimba ni yake, walitaka pia kujua ana msimamo gani na Zari maana kila kukicha wanasikia mambo tofauti katika mitandao na vyombo vya habari,’’ kilisema chanzo hicho.
SABABU ZAZIDI KUANIKWA
Chanzo hicho kilipobanwa na mwanahabari wetu kuhusiana na sababu zilizowafanya ndugu wa Diamond watilie shaka mimba hiyo, kilisema ni kauli ambazo ziliwahi kusemwa na aliyekuwa mpenzi wake Penniel Mungilwa ‘Penny’ na aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga.
“Walishitushwa na kauli ambayo aliwahi kuitoa Penny kwamba Diamond hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba lakini kama hiyo haitoshi, waliitafakari kauli ya mume wa Zari ambaye alidai Zari hawezi kumzalia Diamond ndiyo maana wakataka wapate uhakika,” kilisema chanzo hicho.
MUAFAKA WA KIKAO
Chanzo hicho kikizidi kumwaga ubuyu mbele ya kinasa sauti cha Risasi Mchanganyiko kwamba, baada ya Diamond kubanwa na nduguze, alithibitisha kuwa Zari ndiyo kila kitu kwake kwa sasa, hivyo wasiwe na shaka yoyote juu ya kiumbe kinachotarajiwa kuzaliwa.
“Diamond aliwahakikishia kwamba mzigo ni wake, na msimamo wake ni kufika katika hatua ya ndoa Mungu akijalia.
KUMVISHA PETE
“Kuonesha yupo serious baada ya Diamond kuwatoa hofu ndugu zake, alisema atafanya sapraiz siku ya Mei Mosi katika shoo ya mrembo huyo, All White Party itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar,” kilisema chanzo hicho na kudokeza kuwa Diamond atamvisha pete mrembo huyo.
DIAMOND AFUNGUKA
Ili kuweza kupata ukweli, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond ili aweze kuweka wazi juu ya kikao hicho na kama ni kweli anatarajia kumvisha pete Zari. Diamond alifunguka:
“Yeah ni kweli ndugu zangu walikuwa na shaka lakini nimewahakikishia kwamba kiumbe kilichomo tumboni mwa Zari ni mali yangu, kuhusu kumvisha pete ni mapema kidogo kulizungumzia lakini watu wahudhurie kwa wingi katika shoo ya Zari White Party Ijumaa hii pale Mlimani City kwani nimeandaa sapraizi nyingi sana.
“Mei Mosi itakuwa ni siku ya kihistoria sana kwake kwani kuna mambo muhimu mengi natarajia kumfanyia mpenzi wangu Zari, watu watajua rasmi nia yangu kwa Zari maana ni mwanamke ambaye ameamua kujitoa kwa ajili yangu, hivyo sina budi kumuonesha upendo stahiki, nitafanya kila linalowezekana kumuonyesha namna gani nampenda.”
SHOO YA KIHISTORIA
Kwenye shoo hiyo ya Zari, watu mbalimbali mashuhuri wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo dairekta mkubwa Afrika, Godfather wa Afrika Kusini na Top Ten ya Washiriki wa Shindano la Big Brother ‘Hot Shot’ 2014.
GPL WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment