Huenda hii inatokana na mapenzi yake ndani ya klabu yake ya Manchester United, habari mpya ni kuhusu winga wa klabu hiyo Ashley Young.
Ametoa kauli ambayo pengine ni ngumu
kutolewa na mtu yoyote baada ya kusema yupo radhi kukatwa mshahara wake
ili mradi tu aendelee kubaki kuitumikia klabu hiyo msimu mwingine.
Young amekuwa sehemu ya mafanikio ya
klabu hiyo baada ya kuonekena kurejesha kiwango chake na huenda
akarudishwa katika timu yake ya Taifa lake England.
Man United ilifanikiwa kuizidi ujanja Liverpool kupata saini ya Young akitokea Aston Villa kwa dau la pauni milioni 17 mwaka 2011 na kumpa mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment