Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Naziz: Nadra Kuona Msanii wa Kenya Katika Mabango Barabarani kama ilivyo Bongo

Naziz: Nadra Kuona Msanii wa Kenya Katika Mabango Barabarani kama ilivyo Bongo

Tumezoea kuona wasanii mbalimbali wa Tanzania wakipata ‘endorsement deals’ za makampuni na picha zao kutumika kwenye mabango makubwa ya matangazo barabarani, kitu ambacho kwa mujibu wa Naziz ni nadra kukiona nchini Kenya.

Rapper huyo wa Kenya, Naziz amesema kuwa anaamini kuwa Tanzania ndio inaongoza kufanya vizuri kwenye sanaa ya muziki ikifuatiwa na Uganda na ya tatu ni Kenya.

Naziz ambaye yupo nchini amesema kinachosababisha sanaa ya muziki Kenya ikue taratibu ni kukosekana kwa umoja pamoja na support ya kutosha kutoka kwa makampuni.

“Nadhani nyie ndio mnaongoza kwenye hiyo sekta (muziki),” Naziz ameiambia XXL ya Clouds Fm. “Sio rahisi Kenya kwenda barabarani na kukuta msanii kwenye mabango makubwa, kwasababu corporate haisupport muziki wa Kenya, ni tofauti na hapa corporate ina support.”

“Naweza kusema Kenya tulianza vizuri sana tulikuwa miongoni mwa wale wa mwanzo Afrika mashariki kuwa na endorsements, lakini imefika sehemu kwasababu hakuna umoja…ndio sababu industry ya Kenya imestop kidogo kukua.”

Rapper huyo wa Necessary Noise ameongeza kuwa wasanii wanaochipukia Kenya wanapata ugumu kutokana na matatizo yaliyopo kwenye industry yao.

“Hatuna msanii mkubwa wa Kenya mpya ambaye ametoka ndani ya miaka sita iliyopita hamna, watu wanaoushikilia muziki ni wale wale waliokuwepo.” WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips