Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Kutokana na Kutoa Kichapo Kila Mara Kwa Mpenzi Wake, Daktari Asema Shilole ni Mgonjwa

Kutokana na Kutoa Kichapo Kila Mara Kwa Mpenzi Wake, Daktari Asema Shilole ni Mgonjwa

Shilole
Daktari mmoja bingwa wa saikolojia, Erick Mutchumbh, amesema tabia zinazofanywa na nyota wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ zinaashiria kuwa ni mgonjwa aliyeathirika kisaikolojia na matatizo ya unyanyaswaji wakati wa utoto wake.

Mutchumbh alitoa maelezo hayo baada ya kuombwa kuzungumzia tabia za Shilole za kugombana mara kwa mara na mpenzi wake, Nuh Mziwanda, kama zinaweza kuwa ni tatizo la kisaikolojia linalomsumbua mmoja wao au ni ugomvi wa kawaida wa kimapenzi.

“Mtu yeyote aliyepitia matatizo hasa unyanyasaji akiwa mtoto ‘child abuse’ iwe kunyanyaswa kwa kubakwa, kupigwa, kunyimwa chakula au mateso ya aina hiyo, akikua bila kupata tiba ya kisaikolojia huwa na tatizo kubwa kwa miaka mingi akiwa mtu mzima.

“Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na kupenda kujitenga, hasira za karibu, tabia za ajabu na kubwa zaidi ni kumfanyia mtu mwingine hasa mtoto ukatili aliofanyiwa yeye kitaalamu wanaita ‘Propensity Victimization,’” alisema daktari huyo.

Alisema katika nchi zilizoendelea, tatizo hilo hupewa kipaumbele katika matibabu kuliko ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika kwani madhara yake huwa ni pamoja na mwathirika kuamua kujinyonga au kuua.

Kwa maelezo hayo, mengi yanaonekana kufanana na matukio yaliyowahi kumkuta Shilole, kwani akiwa na umri wa miaka 14, aliwahi kubakwa, pia anatajwa kujihusisha kimapenzi na watu wenye umri mkubwa, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi ngumu katika umri mdogo. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips