Kocha wa klabu ya Arsenal ya uingereza Arsene Wenger amekiri kuwa timu yake ilivurunda na kuiruhusu Everton kuipiku katika nafasi ya nne.
Wenger anasisitiza kuwa timu yake haina budi kufuzu
kwa mashindano ya kombe la mabingwa barani Ulaya mwakani.
Taarifa zinazohusiana
Michezo
Kocha huyo ambaye ameiongoza Arsenal Kufuzu kwa makala 16 ya Kombe la mabingwa barani Ulaya ansema ni bora kwa timu hiyo yenye tajriba kubwa barani kuchuana dhidi ya vilabu vyenye sifa kama yake.
Arsenal itafaidika kwa kuchuana dhidi ya Barcelona , Bayern Munich na Real Madrid katika ligi ya mabingwa kuliko timu zinazoshiriki ligi ya daraja la pili ya Europa.
Ratiba ya Arsenal
Tuesday, 15 April: v West Ham (H)
Saturday, 19 April: v Hull (A)
Monday, 28 April: v Newcastle (H)
Saturday, 3 May: v West Brom (H)
Saturday 11 May: v Norwich (A)
Wenger amekuwa akilaumiwa na mashabiki wa klabu hiyo kuwa amefanya mazoea ya kuridhika na nafasi ya kushiriki mashindano ya kombe la mabingwa pasi na kuingoza timu yake kutwaa taji la ligi ya nyumbani.
Arsenal ilikuwa inaongoza jedwali la ligi kuu mapema mwaka huu lakini ikakumbwa na msururu wa matokeo duni dhidi ya Liverpool Chelsea Manchester na Everton
na sasa imejipata katika hali ya kungangania nafasi ya nne dhidi ya Everton iwapo tu itashinda mechi zake tano zilizosalia.
Arsenal imeratibiwa kuchuaana na West Ham leo jioni katika mechi inayotazamiwa na wengi kuamua iwapo timu hiyo itamaliza katika nafasi hiyo ya nne au la.
The Gunners kwa sasa wanashikilia nafasi ya 5 wakiwa na jumla ya alama 66 mbili nyuma ya Everton .
Liverpool Chelsea na Manchester city zinaongoza kampeini ya kufuzu kwa dimba la mabingwa mwakani katika usanjarihuo.
0 comments:
Post a Comment