Unaambiwa Rais Kagame alimkaribisha Dr. Magufuli kijijini nyumbani kwake na kumzawadia Ng’ombe watano kwa mujibu wa Mwandishi wa habari Kebendera wa Radio na TV ya Taifa Rwanda, ambapo anasema kwa Rwanda ni heshima kubwa sana unapozawadiwa Ngo’mbe.
Rais Magufuli na Rais Kagame nyumbani kijijini kwa Rais Kagame nchini Rwanda, picha imepigwa na ofisi ya Rais Rwanda.
Kabendera anasisitiza zawadi ya Ng’ombe ni zawadi yenye thamani sana nchini Rwanda, kugawiana Ng’ombe ni kitu kimekuwepo toka enzi za mababu, mtu anayekuzawadia Ng’ombe ni mtu anaekupenda sana na kukuheshimu, Wanyarwanda wameitafsiri hii kama undugu na urafiki tofauti na anavyofanya Rais Kagame kwa Marais wengine.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment