Taarifa za mlipuko mkubwa kutokea katika mji wa bandari ya Tianjin,China jana usiku zimeingia kwenye headilines.
Vyombo vya habari vya China vimeripoti kuwa mpaka sasa watu 50 wamepoteza maisha wakiwemo 12 kutoka kikosi cha uokoaji cha nchi hiyo.
Mlipuko huo ulitokea katika mji wa Tianjin-ambao ni mji wa Bandari kuu na sehemu ya viwanda katika eneo la Kaskazini mwa mji mkuu Beijing pia unadaiwa kuwajeruhi mamia ya watu ingawa mpaka sasa idadi kamili haijulikani.
Shirika la habari la Xinhua limesema mlipuko huo ulisababishwa na kemikali zilizokuwa zimehifadhiwa katika bohari moja katika bandari hiyo.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment