Taifa langu Tanzanzia tunahitaji katiba mpya itakayoruhusu Rais kupandishwa kizimbani kwa kutumia mamlaka vibaya (Kufuja mali za umma) mambo ya kuwafanya marais kuwa ni watu wasiyogusika ni mambo ya kikoloni sana.
Tuitafuteni haki ya kupata katiba mpya itakayo wawajibisha Marais ama wakiwa madarakani ama nje ya Madaraka.
Vile vile tuwe na Katiba itakayomfanya Rais kuwepo bungeni na siyo utaratibu wa Sasa Wa Rais kulihutubia Bunge kisha mambo mengine yote anamuachia Waziri mkuu, Hapa hatuwafanyii Wananchi mazuri,Kumbuka Waziri huyu alichaguliwa na jimbo moja sasa anakuja kujibu Maswali ya nchi nzima....Tubadili muelekeo wa kisiasa kama tunataka kuwaletea Watanzania maendeleo na siyo maigizo ya kisiasa.
Kwasasa ni lazima waliyopo madarakani mkubali kupoteza vitu fulani na kuongeza vitu fulani vyenye manufaa kwa Wananchi....
TUITAFUTENI KATIBA MPYA
Written by Henry KilewoWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment