Rais anashangaa kwanini mikutano ya afrika ya mashariki ifanyike kwenye hoteli ya Ngurdoto wakati kuna ukumbi wa AICC ambao hauna gharama kama zinazotozwa na hoteli ya hadhi ya Ngurdoto. Rais Kenyatta aliinamisha kichwa huku akicheka, wajumbe wote kwenye ukumbi wakauelewa ujumbe wa ubanaji wa matumizi.
Lakini ni Ngurdoto hii hii ambayo wakati awamu ya nne inaanza kazi, ilihodhi semina elekezi, ambayo ilitumia fedha nyingi. Sina uhakika, nadhani kwamba mmiliki wa hii hoteli atakuwa ni mmoja wa vigogo wa nchi hii, hivyo tenda za uhakika kama vile semina elekezi na mikutano ya east africa, huwa ni kipindi cha neema.
Sekretarieti ya east african community imekumbushwa kuwa watu wa ukanda huu ni masikini, hivyo wasipende anasa za ajabu ajabu. Ni ujumbe mzuri, ila mmiliki wa hoteli ya Ngurdoto atauchukia sana uongozi mpya wa Rais Magufuli ndani ya jumuia ya afrika ya mashariki, katangaziwa njaa tangu mapema kabisa. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment