Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Nay wa Mitego Adai Hela Pamoja na Mali Anazomiliki Zina Thamani ya Bilioni Moja

Nay wa Mitego Adai Hela Pamoja na Mali Anazomiliki Zina Thamani ya Bilioni Moja

Nay wa Mitego Akiwa na Gari yake
Staa wa muziki Nay wa Mitego amedai kuwa hela anazomiliki benki pamoja na mali anazomiliki zina thamani ya bilioni 1.

Akizungumza katika kipindi cha Weekend Chat Show cha Clouds TV Ijumaa hii, Nay alisema biashara pamoja na muziki wake ni vitu vinavyomwingizia pesa nyingi.

“Mimi mali zangu na kila kitu zinafika kwenye bilioni hivi, ukichanganya hela zilizo benki pamoja na biashara ninazofanya thamani yake zinafikia bilioni moja na kitu. Sitaki kudanganya watu sijui kwenye bilioni 2 huko,” alisema Nay.


Nay alisema hela hizo amezipata kupitia biashara ya daladala pamoja na muziki wake.

Rapa huyo mwaka 2014 alihamia kwenye nyumba yake iliyopo Mbezi jijini Dar na kudai nyumba hiyo ina thamani ya milioni 200.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips