Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza
kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya
Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro
mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo
vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema
jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali
hiyo majira ya saa nane na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea
hospitali nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma,
hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa
maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga
chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya
mapungufu yaliyopo.
“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi
kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa.
Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza
Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa
Hospitali hiyo.
Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa
siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi
cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka
hatarishi za hospitali hiyo.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo
alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa
kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka
mitatu na nusu.
Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya
chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia
mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza
ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka
kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna
mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.
Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa
hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha mapungufu
yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio
hilo.
Tazama MO tv, kuangalia tukio hilo hapa:
Imeandaliwa na Magreth Kinabo, (MAELEZO), Andrew Chale, Modewjiblog/MO tv)
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati)
akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya
Sanitas, Bi. Gean Cabral wakati walipowasilia katika ziara hiyo..
Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.
Dk.
Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna
Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa
ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa
Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral
Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya
'karatasi' iliyoandikwa ujumbe mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa
wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..
Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya
Maabara ya Hospitali hiyo licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini
imeshindwa kuweka mpangilio mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara.
ikiwemo suala la usafi
Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla
(kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine
akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia)
wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya
kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya,
zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. (Picha zote na Andrew
Chale,Modewjiblog/MO tv).
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment