Sasa hivi imekuwa fasheni wabunge wetu kukamatwa hasa maeneo niliyotaja kwenye uchaguzi ambao ni dhahiri Ukawa wana uwezo wa kupata meya.
Ajabu viongozi wa juu mko kimya kwa nini? Mumechoka na kuona bora liende? Wananchi ndio waliowachagua madiwani kwa nini wanyimwe haki yao ya kuongoza hizo halmashauri?
Nawashauri muitishe press tena live coverage kwenye Tv zetu na kutueleza kwa nini wabunge wetu wananyanyasika kiasi hiki?
Hivi kweli miaka ijayo watu watajitokeza kugombea kwa vyama vyetu kama mateso ndio haya?
Kimya chenu kinatutia hasira sana na sisi hatuwezi kukubali unyonge huu abadani.
PSE haraka sana tuambieni na taifa lijue maana wapo wanaoaminishwa kuwa wabunge wa Ukawa ni wakorofi na kupoteza maana ya wanachopigania.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment