Mwigizaji wa Hollywood, Marekani, Lupita Nyong’o aliweka headlines kubwa sana Africa na dunia nzima baada ya staa huyo kucheza movie iliyoingiza mamilioni ya faida kwenye movie Industry ya Hollywood, 12 Years A Slave, movie ambayo pia ilimuwezesha Lupita kupata tuzo ya Oscars mwaka 2014 kama Best Supporting Actress.
Nimekutana na interview moja aliyofanya Lupita Nyong’o
na ndani yake amezungumzia vitu vingi ikiwemo, ilikuwaje akapata nafasi
ya kucheza script ya movie hiyo na kama ana mipango ya kuja kucheza
movie itakayopita kiwango chake kwenye 12 Years A Slave?
Kuhusu kupata nafasi ya kucheza script ya movie ya 12 Years A Slave, Lupita Nyong’o alisema…
>>> ” nilisikia
kuhusu auditions za movie hiyo sema sikuwa New York so nikaipotezea,
lakini manager wangu D.D Ray alifanikiwa kuipata ile script kwa ajili ya
mteja wake mwengine ndipo alipo kutana na “Patsey” character ambaye
alihisi nitaweza kumcheza… nikarekodi mkanda ya kwanza ya role hiyo na
ikatumwa kwa manager wangu wa New York, baada ya wiki moja nikaitwa New
York kwenye auditions za mwisho na baada ya kukaa kwa saa nzima kwenye
foleni nikafanikiwa kupita, na wiki mbili baadae nikapigiwa simu kwenda
kukutana na producer wa movie ili kuanza rasmi…“<<< Lupita Nyong’o.
Badaae Lupita akaulizwa kama atakuja kucheza movie itakayovuka kiwago chake kwenye movie ya 12 Years A Slave movie iliyomuwezesha apate tuzo kubwa ya Oscars, msanii huyo kutoka Kenya alikuwa na haya ya kusema…
>>> ” Sijui
kama kuna movie nitakayokuja kucheza ikavuka levo ya 12 Years A Slave,
sidhani! Movie ya 12 Years A Slave ipo kwenye levo ya juu sana, stori
yake iligusa wengi duniani na imenifungulia milango mingi… lakini kuja
kucheza movie ya kuzidi kiwango kile haitokuja kutokea kwa sababu
experience niliyoipata ni ya kipekee sana, japo nataka kucheza role
tofauti za movie na pia kujaribu character tofauti, na ninashukuru kwa
sababu sasa hivi nimepata fursa ya kufanya hivyo na kutanaua kipaji
changu...” <<< Lupita Nyong’o.
Ukiacha 12 Years A Slave, movie nyingine zilizochezwa na Lupita Nyong’o ni pamoja na; Star Wars Episode VII – The Force Awakens inayotegemea kuwa sokoni tarehe 15 December 2015 na The Jungle Book inayotegemea kutoka tarehe 07 April 2016.
0 comments:
Post a Comment