Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Lazaro Mambosasa alisema kuwa Octoba 26, majira ya saa tisa mchana katika kijiji cha sokoni,Kata ya Sirari,Wilayani Tarime Gari lenye namba za usajili T.562 CAP aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Joseph Magazin ikitokea katika kituo cha mabasi cha Sirari kuelekea katika egesho la kituo cha mafuta ilipigwa mawe .
Mambosasa alisema gari hilo lilishambuliwa kwa kurushiwa mawe na kuvunjwa kioo cha mbele,vioo vine vya madirisha upande wa kulia na vioo vitatu vya madirisha upande wa kushoto vyote vikiwa na thamani ya 6,500,000.
Aliongeza kuwa siku hiyohiyo majira ya saa sita mchana gari lingine lenye namba za usajili T.925 CZM aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Ezekia Merico(32) Dereva mkazi wa Isamilo Mwanza ilishambuliwa kwa mawe na kuvunjwa kioo kimoja cha Dirisha la nyuma upande wa kulia lenye thamani ya 2,000,000.
Mambosasa alisema kuwa Magari hayo ni mali ya Kampuni ya Zakaria Express,nakwamba watuhumiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambao ni Libaya Msabi (34)mkazi wa Remagwe na Marwa Juma(17) mkazi wa Sokoni Sirari nakwamba
Quote: What we have, what we wish we had - ambitions fulfilled, ambitions disappointed, investments won, investments lost, elections won, elections lost - these things may occupy our attention, but they do not define us. By Mitt Romney WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment