Kwanza tukubali matokeo!, yawe ni ushindi halali au ndio matokeo ya bao la mkono, the end justify the means, tukubali matokeo kwa roho safi, roho nyeupe, japo we are very bitter!, Mungu ametupa amri kuu kuliko zote ni mapendo!. Tukubali kushindwa, tuwapende washindi, tukubali matokeo na tuwapongeze Washindi.
Tusianze kumtafuta mchawi kwa kunyoosheana vidole kuhusu sababu za kushindwa, tukubali tuu kuwa haya ndio matokeo, tuufunge ukurasa wa uchaguzi huu kwa amani, tuufungue ukurasa mpya wa maisha baada ya uchaguzi.
Pamoja na UKAWA kupoteza ushindi wa jumla, na kupoteza baadhi ya majimbo, lakini mavuno ni makubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote, hivyo UKAWA ime gain na CCM ndio ime loose!.
Ukiwa na kondoo 100, ukampoteza kondoo mmoja, mchungaji mwema atawaacha wale kondoo 99, kwenda kumrudisha kondoo mmoja aliyepotea, na akimpata itakuwa ni furaha kubwa!.
CCM ilikuwa na majimbo mengi zaidi wakati inaingia uchaguzi huu, lakini itatoka imejeruhiwa vibaya kwa kupoteza majimbo mengi na viti vingi vya udiwani!.
Mzee wetu ENL, Chadema na wana UKAWA, tuwe na shukrani kwa kodogo tulichokipata, UKAWA ndio the gainers na CCM ndio the loosers.
There is life baada ya uchaguzi, hivyo sasa ni wakati wa kuendelea na maisha yetu ya kawaida!.
Tulidhamiria, tukajaribu, tukatekeleza, tukapiga kampeni, tukapiga kura, tuwawachagua viongozi wetu, lakini kura zetu hazikutosha!.
Wa kupeana pole!, tupeane pole, na wa kuwapongeza, tuwapongeze!.
By Pasco/Jamii Forums
Quote: What we have, what we wish we had - ambitions fulfilled, ambitions disappointed, investments won, investments lost, elections won, elections lost - these things may occupy our attention, but they do not define us. By Mitt Romney WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment