Bado mambo sio mazuri kwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ambaye anahusishwa kufutwa kazi klabuni hapo kufuatia mwenendo mbovu wa klabu hiyo. Stori za Mourinho kufutwa kazi zimeandikwa na magazeti mengi ya Uingereza ya October 26, hata hivyo akiwa katika wakati mgumu kwa sasa Shirikisho la soka Uingereza limetangaza kumshitaki Mourinho.
Shirikisho la soka Uingereza FA limetangaza kumshitaki kocha huyo kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha kwa muamuzi wa mehi ya Chelsea dhidi ya West Ham United. Mourinho aliamuliwa na muamuzi Jonathan Moss kutoka katika benchi kutokana na kauli alizokuwa anazitoa mbele ya refa huyo wakati wa mapumziko.
Awali Mourinho
alipigwa faini ya pound 50,000 na kufungiwa mchezo mmoja baada ya
kutenda kosa la kutoa kauli mbovu kwa muamuzi wa akiba, hii ilikuwa
katika mechi dhidi ya Southampton October 3 ambapo Chelsea ilipoteza mchezo huo, licha ya kuwa Mourinho alikata rufaa kwa kosa hilo October 26 FA wametangaza tena kumshitaki Mourinho kwa tabia hiyo na huenda akakumbana na adhabu kali kutoka FA.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment