Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Vitu vitano ambavyo huenda hauvifahamu kuhusu maisha ya Cristiano Ronaldo…

Vitu vitano ambavyo huenda hauvifahamu kuhusu maisha ya Cristiano Ronaldo…

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ambaye amewahi kuitumikia klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa zaidi ya miaka mitano. October 26 naomba nikukumbushe vitu vitano ambavyo huenda hauvifahamu kuhusu maisha yake.
1- Aliwahi kufukuzwa shule baada ya kumrushia kiti mwalimu wake wa shule, kitu ambacho Ronaldo anasema alifanya vile kwa sababu mwalimu wake alimvunjia heshima.
ronaldochild5
2- Huenda hili likawa geni kwako Cristiano Ronaldo ambaye ni raia wa Ureno pamoja na wazazi wake, kwa upande wa mama yake ana asili ya Afrika. Bibi wa mama yake Cristiano Ronaldo alikuwa ni mtu mwenye asili ya Cape Verde.
871-cristiano-ronaldo-picture-next-to-his-mother
3- Kama ambavyo tumezoea kuishi maisha ya watoto wa kiume na wakike kulala vyumba tofauti, kwa upande wa Cristiano Ronaldo aliwahi kulazimika kulala chumba kimoja na dada zake kwa sababu ya umasikini wa familia yake wa kushindwa kumudu kupanga nyumba kubwa.
871-cristiano-ronaldo-family-mother-father-and-sisters
4- Licha ya kuwa ni staa wa soka lakini hadi leo hii mwanamke aliyemzaa Cristiano Ronaldo Junior ambaye ni mtoto wa Ronaldo hajulikani, jambo hili linawashangaza wengi kwa mtu maarufu kama Ronaldo watu kushindwa kumjua mzazi mwenzake.
Cristiano-Ronaldo-with-son-Cristiano-Jr-Picture
5- Baada ya fainali za Kombe la 2006 aliomba kuondoka Man United baada ya kugombana na Wayne Rooney katika michuano ya Kombe la Dunia 2006, hivyo Wayne Rooney akaoneshwa kadi nyekundu. Tukio ambalo lilivunja mahusiano mazuri ya baina ya wachezaji hao.
Cristiano Ronaldo
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips