Post hii ni maalum kwa staa wa muziki wa Kenya anaetajwa kuingia kwenye
TOP 5 ya Wasanii matajiri wa muziki wa kizazi kipya Afrika Mashariki
huku orodha hiyo ikiwa na watu wengine kama Jose Chameleone.
Imefahamika kwamba Jaguar alikataa kuja kwenye tuzo za Kili 2014
alizokua nominated baada ya waandaaji kushindwa kufikia masharti
aliyowapa na badala yake akaamua kwenda kuhudhuria harusi ya producer wa
DNA aitwae Refigah.
Jaguar alitaka atumiwe ticket ya ndege ya business class, alitaka
achukuliwe chumba kwenye hoteli ya nyota tano, apewe ulinzi popote
atakapokwenda na vilevile apewe gari zuri la kifahari la kutembelea.
Kwenye sharti jingine Jaguar alitoa option kwa waandaaji na kuwaambia
kama wangeshindwa kumpa ticket ya ndege basi walipaswa kuweka mafuta ili
aje na ndege yake ndogo anayomiliki.
Alipohojiwa na ghafla.co.ke Jaguar alisema asingeweza kuhudhuria tukio
ambalo asingepewa heshima aliyoitaka kama ambavyo huwa anaipata
anapokwenda kwenye nchi nyingine katika matukio kama haya ndio maana
ilikua bora ahudhurie harusi na kuongeza kwamba ‘nitahudhuria iwapo
wataanza kuwa-treat vizuri wasanii wa Kenya’
Tuzo za KILI 2014 zilihudhuriwa na mastaa wawili wa Kenya ambao ni Wyre
na Amani huku Uganda ikiwakilishwa na Jose Chameleone ambae ndio
alitangazwa mshindi kwenye kipengele cha Afrika Mashariki.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment