Manchester United imemsajili winga wa PSV Memphis Depay kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu na huenda ikamtema mchezaji wao Angel Di Maria.
Lakini klabu ya Paris Saint-Germain
‘PSV’ ya Ufaransa imesema ipo tayari kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo
kama ataruhusiwa na uongozi wa timu yake ili kwenda kuongeza nguvu
kwenye kikosi chao.
Mchezaji huyo alisajili kwa pauni milioni 60 akitokea Real Madrid lakini hakuonyesha kiwango kizuri msimu huu na kuwa hatarini kutemwa.
Man United awali ilitaka kumuuza mchezaji huyo lakini baadaye meneja wa timu hiyo Luis Van Gaal alibadili mawazo na kudai ataendelea kubaki kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mwingine.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment