H: Baba amesajiliwa na klabu ya Toto African ya jijini Mwanza hali inayomfanya kuwa mbali na familia yake ambayo ipo jijini Dar,na ndiyo sababu kubwa iliyotajwa kukatazwa na mkewe kuichezea timu hiyo.
Kwa mujibu wa msanii huyo alisema kuwa mkewe alikaa kikao na ndugu zake waliopo jijini Mwanza kuzungumzia suala hilo kama atakubali abaki kucheza mpira atacheza lakini akibaki na msimamo wake basi ataacha kucheza na kurudi Dar.
‘’Unajua wife anacholalamika kuwa nitakuwa mbali na familia kwahiyo atakosa haki yake ya msingi kama mke,’alisema H: Baba. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment