Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » January Makamba Kaharibu Utamu wa Hotuba kwa Kusema Uongo

January Makamba Kaharibu Utamu wa Hotuba kwa Kusema Uongo

Nimemsikiliza Januari Makamba wakati akitangaza nia, amezungumza mambo mengi lakini ameharibu utamu wa hotuba hiyo kwa kusema uongo.

Makamba katika hotuba yake amesema itachukua miaka mingi hata kumi kwa Tanzania kuanza kuvuna gesi na rais ajaye anaweza akaondoka madarakani bado gesi haijaanza kutumika.

Huu ni uongo wa wazi ana pengine inaweza kuwa ni kutojua kwamba tayari gesi imeanza kutumika kwenye maeneo mengi ikiwemo kweye viwanda mbalimbali hususani kwenye jiji la Dar es Salaam na kuna maeneo mengine kwenye majumba inatumika.

Namshangaa Januari anaposema gesi haitotumika kwa miaka ya karibu, anataka kutuambia hata mioundo mbinu ya gesi iliyojengwa itaanza kufanya kazi baada ya miaka kumi?

Namshauri aache kuzungumzia mambo ambayo hayajui na kama anatamani kuyazungumzia basi angeuliza kwa wataalamu wa masuala ya gesi kabla ya kufungua mdomo kuongea asiyoyajua.

Kwa mujibu wa wizara ya nishati na madini gesi itaanza kutumika miezi michache ijayo na tayari mabomba ya gesi yamekamilika kwa asilimia 90 na hata kiwanda cha DANGOTE kinachojengwa kitatumia gesi hiyo ambapo kiwanda hicho kitaanza uzalishaji mwezi wa nane kwa maana hiyo gesi itaanza kutumika kabla ya kiwanda hicho kuanza uzalishaji, WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips