Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mafuriko ya Ghana yaliyoua watu 175,yamkumba Van Vicker akiwa njiani kuelekea kwake

Mafuriko ya Ghana yaliyoua watu 175,yamkumba Van Vicker akiwa njiani kuelekea kwake

Mafuriko makubwa yaliyoikumba jiji la Accra nchini Ghana usiku wa kuamkia juzi na kuleta maafa ya kuua watu 175 wakiwa wamejihifadhi kwenye kituo cha mafuta baada ya kituo hicho kulipuka moto,yamemkumba pia Staa wa filamu nchini humo Van Vicker akiwa barabarani akielekea nyumbani kwake.

Kupitia akaunti yake Instagram Van Vicker aliandika kuwa ameshuhudia mafuriko kwa macho yake (live),huku taa za barabarani zikiwa haziwaki,kuna mashimo,matakataka,umeme ukiwa umekatika na barabara zilikuwa zimefurika maji, na magari yalikuwa yameharibika.

Pia aliongeza kuwa waliokuwa wakitembea barabarani walikuwa wakitafuta pa kujihifadhi,madereva walipaniki na bado wakati huo mvua ilikuwa ikinyeesha na pia foleni ilikuwa kubwa na barabara ni ndogo.
Ambapo alisema kuwa kawaida huwa inamchukua dakika 45 kwenda nyumbani kwake lakini siku hiyo ilimchukua masaa sita kufika nyumbani kwake. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips