Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Sitti Mtemvu kuzindua Kitabu cha 'Chozi la Sitti' Akielezea Faida na Hasara za Mitandao ya Kijamii

Sitti Mtemvu kuzindua Kitabu cha 'Chozi la Sitti' Akielezea Faida na Hasara za Mitandao ya Kijamii

Taarifa ya aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, kwa vyombo vya habari leo imeeleza kuwa, Sitti atazindua kitabu kinachoelezea faida na hasara ya mitandao ya kijamii.

Amesema pamoja na kwamba mitandao ya kijamii ikitumiwa vizuri, huleta mapinduzi ya kimaendeleo ya kihabari kwa haraka.

Amesema maudhui yaliyopo katika kitabu hicho ni yanamlenga yeye moja kwa moja kama mhusika na kwamba pamoja na maumivu na athari azipatazo mhusika kitaelezea ni kwa jinsi gani ataweza kujifunza na kunyanyuka upya.

Mei 2, 2015 mwaka huu pia uzinduzi wa kitabu hicho utaenda sambamba na uzinduzi wa 'Taasisi ya Sitti Tanzania' yenye lengo la kusaidia watu wenye shida na kuweza kuendeleza gurudumu la maendeleo Tanzania.

Itakumbukwa sakata la Sitti kudaiwa kuwa ameghushi cheti cha kuzaliwa liliibuka kwenye kwa kasi mwaka jana kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyozifanya mamlaka husika kuanza kufuatilia uhalali wa cheti chake cha kuzaliwa....hadi pale alipojivua taji alilokuwa amevishwa baada ya kushinikizwa na watu mbalimbali kuwa aachie taji hilo kwa kile kilichoitwa ni kukosa uaminifu na kukosa sifa ya kushikilia nafasi hiyo. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips