Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Simba Wamesema Haya Baada ya Ramadhani Singano Kusajiliwa na AZAM Siku Moja Baada ya Kusinda Kesi

Simba Wamesema Haya Baada ya Ramadhani Singano Kusajiliwa na AZAM Siku Moja Baada ya Kusinda Kesi

Baada ya aliyekuwa winga wa Simba Ramadhani Singano ‘Messi’ kumwaga wino wa kukitumikia kikosi cha ‘wanalambalamba’ Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili, klabu yake ya zamani (Simba) imesema dili hilo lilipangwa na Azam ili mkataba wa mchezaji huyo na klabu ya Simba uvunjwe na wao wamnase kirahisi.

Afisa habari wa Simba Hajji Manara amesema Azam walipanga jambo hilo kwasababu Singano alishasema kwenye kikao cha kwanza kuwa Azam ni miongoni mwa klabu ambazo zilikuwa zikimuhitaji wakati bado akiwa na mkataba na Simba.

“Hili jambo limepangwa, na mkiuliza nani amelipanga mnamajawabu. Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji juzi imemtangaza Messi ni mchezaji huru wamevunja mkataba wetu, leo amesaini Azam. TFF hawajatuletea barua, huyu mchezaji mpaka juzi sisi tunatambua ni mchezaji wa Simba mpaka hivi sasa barua ‘official’ haijaja ndio maana nasema hili jambo lilipangwa sikunyingi na TFF wanalijua hili”, amesema Manara.

“Itawezekana vipi mchezaji ambaye sisi barua hatujapata ya kuvunjwa kwa mkataba wake asaini kwenye klabu nyingine? Kwakutopewa barua mpaka leo maana yake nini? Sisi tunashindwa kutoa ‘official statement’ ya klabu na tunashindwa kuchukua hatua zozote wakati hawajatuletea barua tayari mchezaji kaenda Azam”, Manara alihoji

“Na kwenye kikao aliwataja Azam kuwa ni miongoni mwa klabu ambazo zilikuwa zinamsumbua”, alimaliza.

Leo mchana Singano amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu ya Azam FC baada ya mkataba wake na Simba kuvunjwa na kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji kufuatia Simba kushindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vya mkataba kati ya mchezaji na klabu.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips