Ok hayo yakapita ikaja 2005, nikaletewa malaika mwenye sura nzuri kutoka Msoga hana kitu chochote zaidi ya sura yenye mvuto. Akaja na ahadi kemkem za maisha bora kwa kila mtanzania lakini baada ya miaka mingine 10, amefanikiwa kutimiza hiyo ahadi kwa familia yake tu, taifa zima bado tunasubiria hizo ahadi. Tumeshuhudia mambo ya ajabu kama escrow, utapeli kwenye bomba la gesi na mikataba ya kuchimba madini, gesi, nk.
Safari hii sifanganyiki, hawa ninaoletewa wanaoitwa wasafi halafu nikishawapa kura yangu wananiliza, wanasema kwamba kwa miaka yote 10 waliwasahau wazazi wangu wakulima, wanachomoka na mali zangu mimi mpiga kura, halafu hawataki hata niwaulize chochote.
Safari hii nimebadilisha mawazo. NAMCHAGUA FISADI maana yeye sitamshangaa akiniibia maana mmeshasema kwamba ni fisadi. Naumia sana ninaposhawishiwa kumchagua "msafi" halafu ananiibia. SAFARI HII SIDANGANYIKI, NAMCHAGUA FISADI.
By Mwananchit/JF WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment