Alikiba amekiri kutofurahishwa na uhasama unaondelea kati ya mashabiki
wake na mashabiki wa Diamond Platnumz kwenye mitandao ya kijamii japo
amesema hana uwezo wa kuzuia hali hiyo.
- “Unajua sisi ni vioo vya jamii na tunapendwa na watu wengi sasa
unapoona mambo yanatokea kama hivyo huwezi kufanya chochote na mimi
siwezi kuingilia suala lolote la mashabiki,” Alikiba amekiambia kipindi
cha Leo Tena cha Clouds FM.
- “Lakini kiukweli sifurahishwi nalo kama kuna uwezekano wangeacha tu. Kiukweli tusupport vya kwetu ili tuwende kwenda mbele.”
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment