Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Wanafunzi wa chuo kikuu cha UDSM wagoma kuingia darasani kwa madai ya kutopewa fedha za kujikimu.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha UDSM wagoma kuingia darasani kwa madai ya kutopewa fedha za kujikimu.

Maelfu ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani wameanza mgomo kuingia darasani kwa madai ya kutopewa fedha za kujikimu kwa zaidi ya wiki 11 huku wakitaja gharama za maisha zikiwa zimepanda mara dufu.

Wakiongea katika viwanja vya chuo kikuu jijini Dar es Salaam kwa kile walichokiainisha kuwa ni njaa kali pamoja na kueleza kuendelea na mgomo hadi fedha zitakpoingia kwenye akaunti zao wametaja serikali kuchelewesha fedha hizo kupitia bodi ya mikopo kuwa ni kuwadhoofisha kimasomo.

Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandara pamoja na kukiri madai ya wanafunzi elfu saba kati ya zaidi ya elfu kumi wanaofadhiliwa na serikali kupitia bodi ya mikopo kucheleweshewa fedha zao kuwa ya msingi,amesema tayari amezungumza na bodi ya mikopo ambao wamemwahidi kuleta fedha zao haraka iwezekanavyo na kuwaomba wanafunzi kurejea madarasani kuendelea na masomo.

Wakati huohuo takribani wanafunzi 400 wa chuo kikuu cha Mt. Josephu cha Mbezi jijini Dar es Salaam mwaka wa kwanza wamesimamishwa masomo kwa muda usiojulikana baada ya kugoma kuingia madarasani wakidai fedha za kujikim kutoka bodi ya mikopo tangu mwezi Desemba mwaka jana hadi sasa wakieleza kuishindwa kuendesha maisha yao ya shule na kuhimili mazingira ya kupanga nyumba mitaani.

Katika taarifa ya kusimamishWa wanafunzi hao iliyotolewa na makamu mkuu wa chuo cha Mt.Josephu Bw.Loyola Proteep aliyeambatana na mkuu wa wanafunzi maarufu kama Dean anakiri madai ya wanafunzi hao kuwa ya msingi na kuongeza kuwa waliwaomba utulivu na kuingia Madarasani wakati wakifuatilia madai yao bodi ya mikopo bila ya mafanikio na uongozi kuchukua uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza hadi vikao vya bodi vitakapoamua vinginevyo.

                         Gallos official Blog WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips