Akizungumza na jana baba mzazi wa watoto hao Oturo alisema kuwa anatarajia kuwasafirisha watoto wake ambao ni Sarah David(10) na Goodluck David(04) leo au kesho kuelekea Mkoani Musoma kwa ajili ya mazishi.
Alisema kifo cha watoto wake ni cha utata kutokana na kwamba watoto walikuwa ni wengi katika eneo hilo lakini ameshangaa watoto wake wote wawili kupigwa na shoti ya umeme na wote baada ya hapo walipelekwa katika Hospitali ya TMJ na kuhamishiwa katika Hospitali ya Mwananyamala lakini wote walipoteza maisha.
Akizungumzia suala la ushiriki wa kanisa katika msiba huo alisema kuwa Askofu Gwajima pamoja na waumini wake wanafika nyumbani kwake lakini hawajashiriki kitu chochote.
“Kwa sasa nipo katika maandalizi ya kuwasafirisha watoto wangu kwenda Musoma kwa ajili ya mazishi, ingawaje katika maandalizi yangu Askofu Gwajima na waumini wake hawajatoa kitu chochote kwa ajili yamaandalizi ya safari hii.
“Mimi ninachong’ang’ana ni kuhakikisha kuwa wanangu ninawasafirisha kwenda kuwapumnzisha nyumbani kwetu nilipozaliwa ambako ni Musoma na si vinginevyo,” alisema Oturo.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima alipotafutwa kuzungumzia swala hilo simu yake iliita bila kupokelewa na wakati mwingine ilikuwa ilikuwa haipatikani kabisa.
Pamoja na jitihada za kupiga simu kwa askofu huyo kugongwa mwamba, lakini ilisikika miito ya nyimbo pamoja na mahubiri mbalimbali katika simu yake.
Moja ya muito huo ulisikika ukisema “Biblia ni njia kwa waliopotea, Biblia ni njia kwa waliokata tama, Biblia ni uponyaji kwa wagonjwa, Bibilia ni faraja kwa walio na dhiki,” yalisikika maneno hayo. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment