Hakuna ubishi kua kwa sasa diamond platnumz ndie msanii anae ongoza kupigwa vita kuliko msanii yeyote hapa nchini.
Vita hiyo ina ongozwa na baadhi ya walio wahi kuwa wapenzi wake pia na
mahasimu wake wa kimuziki (wasanii wengine) kupitia mashabiki zao.
Sawa ni jambo la kawaida kwa wasanii wakubwa duniani na mastar wengine
kama wachezaji,maboxer pamoja na waigizaji kuwa na maadui hili
linathibitishwa na mfano wasanii kadhaa wa kimarekani walivyo na maadui
mpaka inafikia kupigana risasi mfano 2pac,BIG,50cent,mayweather na
wengine kibao.
Sababu kubwa za diamond kuanzishiwa vita "maalum" ili ashuke kimuziki na
kimafanikio ni kutokana na maneno ya wengi eti kua
anaringa,anadharau,ana nyodo,ana mamneno ya shombo,ana ropoka sana,mtoto
wa uswahili,hajasoma,mchawi na visababu kedekede.
Wadadisi wa mambo wanasema kua chuki dhidi ya diamond si tu inatokana na
sababu zilizo tajwa hapo juu bali inaenda mbali zaidi mapaka kwa team
nzima ya diamond hasa mameneja wake.
hapa ni kwamba kwa sasa hakuna asie jua kua unapo ongelea mameneja
wakali Tanzania una waongelea Babu tale na Said Fella,Mzozo unakuja pale
ambapo kuna watu wanatamani kufika level za wakina Tale but wana chemka
ndipo wanapo anzisha kampeni ya kuwaharibia hawa jamaa kwa kisingizio
cha kua eti ni wanyonyaji,wana haribu soko la muziki wa bongo fleva na
maneno kibao.
kiukweli hawa watu hawajawahi kushindwa kwenye menejimenti yao,kila
msanii wanae mmeneji lazma afike mbali wangapi wamejaribu wakaishia
njiani? mfano ustadh "juma na musoma",
Kwa hiyo tunapo itizama vita dhidi ya diamond tusidhani tu kua mashabiki
ndio wanao tengeneza hii chuki bali ni mkono wa wadau wakubwa wa muziki
hapa nchini wakishirikiana na media kadhaa kuhakikisha wana wapasua
mashabiki kwa makusudi tu ili watimize malengo ya kuwamaliza wahasimu
wao diamond Fella na babu Tale...!!
Tupingane kwa hoja na sio matusi!!
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment