Siku ya leo itakuwa ina mchanganyiko wa furaha na huzuni kwa mashabiki wakereketwa wa Chelsea, kwa sababu watakuwa wanakabidhiwa kombe lao rasmi lakini pia itakuwa ndio mwisho wao kumuona gwiji wa klabu hiyo Didier Drogba akiwa anaichezea timu hiyo.
Kupitia akaunti yak rasmi ya mtandao wa kijamii wa Instagram – Drogba ametangaza kwamba leo ndio itakuwa siku yake ya mwisho kuitumikia Chelsea dimbani
Drogba anasema amezungumza na Kocha Jose Mourinho kuhusu hatma yake na amemuelewa kwamba angependa kuendelea kucheza soka japo kwa msimu mmoja. Hivyo ili aendelee kupata nafasi ya kucheza anahitaji kwenda sehemu nyingine.
Drogba amewatakia kila kheri mashabiki wa Chelsea na ameahidi kurudi kufanya kazi na klabu hiyo huko mbeleni. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment