Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Lady Naa alisema kuwa alimvumilia Hemed kwa muda mrefu kwani alimpa mzigo huo na kumuomba akaushushe dukani kwa rafiki yake maeneo ya Kinondoni lakini hakufanya hivyo na alipokuwa akimkumbusha alikuwa akimwambia kuwa atampelekea.
“Kila nikikutana naye nilikuwa namuomba anirudishie anasema nifanye lolote na kinachonishangaza amezipeleka wapi maana mle kulikuwa na nguo za kike ambazo nilizitoa Uingereza,” alisema Lady Naa.
Alidai kwamba baada ya kumzungusha kwa muda mrefu ndipo alipoamua kumfungulia kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama, Dar ambapo hadi leo anasakwa. Baada ya habari hizo kulifikia gazeti hili, mwanahabari wetu alimwendea hewani Hemed lakini namba yake haikupatikana hivyo jitihada zinaendelea. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment