Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mkenya Aliyehukumiwa Kunyongwa China Kwa Kusafirisha Madawa ya Kulevya

Mkenya Aliyehukumiwa Kunyongwa China Kwa Kusafirisha Madawa ya Kulevya


Mwanadada mwenye umri wa miaka 26 huenda akanyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa ya kulevya nchini china ambapo Mkenya huyu Floviance Owino, aliyehudumu kama msaidizi wa nyumbani alitiwa nguvuni May 2013 akisafiri kuelekea Beijing kutokea hapa Nairobi.

Afisi ya ubalozi wa kenya nchini Uchina umethibitisha kwamba huenda Floviance akanyongwa mwaka huu baada ya kifungo chake cha miaka miwili kukamilika na haya maneno ni kwa mujibu wa dada yake ambaye ni Judith Owino. Judith anasema hakufahamu kuwa dada yake alikuwa amesafiri kwenda China hadi alipopata habari kutoka kutoka ubalozi wa kenya nchini humo.


Nilifahamu kwa mara ya kwanza kuwa alikuwa China nilipopata simu kutoka kwa ofisi za ubalozi, nlifahamu pia kwamba yuko kizuizini akisubiri kunyongwa, ofisi ya Mashauri ya nchi za kigeni ilinipa habari kuhusu hukumu ya kunyongwa kwa dada na kunipa kibali cha haraka kusafiri kwenda China’

Serikali ya uchina hata hivyo ilimwarifu Judith kwamba alikuwa na muda mfupi kugeuza hukumu hiyo na kuzuia dada yake asinyongwe, walinishauri nitafute wakili hivyo kwa sasa nahitaji visa kwenda china maana mda unazidi kupotea.

Mpaka sasa Judith hajapata fursa ya kuzungumza na Floviance kwani serikali ya china haikukubali hilo lifanyike  ‘nilitamani sana kuongea nae lakini walinikatalia, Floviane ana mtoto wa miaka minne aliyemuacha Kenya baada ya kusafiri kwenda China’

Je unaweza kununua maisha kwa gharama yoyote?? Nawaomba watanzania wenzangu msifinye biashara haramu ya madawa ya kulevya, mkikamatwa mnaweza kupoteza maisha!WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips