Shilole a.k.a Shishi Baby
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza, kitendo cha Shilole kufanya vitendo vya kudhalilisha hadharani, si mara yake ya kwanza kufanyika na Baraza hili lilikwishamwita kumuonya.
Taarifa hiyo inaweka wazi kuwa, msanii huyo atakaporejea nchini, litachukua hatua zifuatazo.
1. Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla
2. Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si sanaa na hakuna uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua.
Msanii huyo pia kwa upande wake anasubiriwa kwa hamu kutolea ufafanuzi wa kile kilichotokea kwa mashabiki wake Afrika Mashariki.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment