Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Afande Selle: Picha niliyopigwa nikiwa na boxer haitonikosesha ubunge wa Morogoro Mjini

Afande Selle: Picha niliyopigwa nikiwa na boxer haitonikosesha ubunge wa Morogoro Mjini

10710737_640005322782747_1419489493188895612_n
Seleman Msindi aka Afande Selle anawania kuwa mbunge mtarajiwa wa jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi cha chama cha ACT Tanzania, na haogopi maneno ya ‘haters’ wanaotaka kukiwekea mchanga kitumbua chake kwa mambo yaliyopita.

Bila shaka unakumbuka ile picha ambayo Afande alipigwa akiwa amevua nguo na kubakia na boxer tu jukwaani wakati akitumbuiza!

Mfalme huyo wa Rhymes anaamini kuwa picha haiwezi kumchafulia CV yake mbele ya waajiri wake watarajiwa aka wananchi wa Morogoro Mjini.

“Hainiumizi, inanifurahisha,” Afande aliiambia 255 ya XXL, Clouds FM.

“Inanifanya nione kama namuenzi ipasavyo mfalme Daudi baba yake Suleiman. Inanifanya niamini kwamba ufalme wangu haukuwa wa kubebwa. Kwahiyo mpaka hapo inaashiria utashi wangu, hadhi yangu na ufalme wangu ambao leo hii unaenda kuwa ubunge wa Morogoro.”

Unadhani Afande anaweza kuwa mbunge mzuri wa Morogoro Mjini? WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips