Watafiti wa Marekani wamebaini kuwa kufanya ngono mara nyingi kunaweza kupoteza uhalisia, mahaba na hamu. Wanadai kuwa mapenzi ni ‘ubora’ zaidi kuliko ‘wingi’ na kwamba kufanya zaidi kunaweza kuwafanya wapenzi kuyachoka.
Watafiti kwenye chuo kikuu cha Carnegie Mellon walibaini mwanzo kuwa ngono na furaha si vitu vya moja kwa moja kama inavyofikiriwa. Kuwa na furaha kwa mfano kunaweza kumfanya mtu kufanya mapenzi zaidi au kuwa na afya kunaweza kusababisha mtu kuwa na furaha na kutaka kufanya mapenzi zaidi.
Kama sehemu ya utafiti huo, wanasayansi waliwafanyia majaribio baadhi ya wapenzi kufanya mapenzi zaidi. Waliripoti kuwa kufanya mapenzi zaidi hakukuwafanya wawe na furaha zaidi kwasababu kuongezeka kwa kufanya kulipunguza hamu na raha ya mapenzi.
Watu 128 waliokuwa na umri wa kati 35-65 waliopo kwenye ndoa (wanawake na wanaume) walishriki utafiti huo. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment