Akizungumza na gazeti la Ijumaa Wikienda, Shamsa alitiririka kwamba mara nyingi alikuwa akichezea kichapo tena akiwa na ujauzito wa miezi minne wa mtoto wao, Terry lakini kipindi chote hicho alikuwa akivumilia ili kukwepa aibu na kumlindia heshima.
“Dick ameninyanyasa kwa muda mrefu lakini kuepuka aibu ya kuwa mastaa hawatulii, nikawa navumilia kipigo kikali hivyo niliamua kuachana naye tangu Oktoba, mwaka jana na sikutaka kusema ila sasa nimeweka wazi kutokana na yeye kuanika mambo yetu kwenye mtandao wa kijamii,” alisema Shamsa.
Alipotafutwa Dick, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment