Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » , , » MBOWE Apigilia Msumari Kauli Ya Mnyika.....Asema Hawatamruhusu Kiongozi wa ACT Zitto KABWE Kujiunga na UKAWA kwa Madai Kuwa Atavujisha SIRI Zao

MBOWE Apigilia Msumari Kauli Ya Mnyika.....Asema Hawatamruhusu Kiongozi wa ACT Zitto KABWE Kujiunga na UKAWA kwa Madai Kuwa Atavujisha SIRI Zao

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema hawatamruhusu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Kauli ya Mbowe imetolewa siku chache baada ya Zitto kutangaza kuwa ACT ipo tayari kujiunga na Ukawa kama wanavyotaka Watanzania wakiwamo baadhi ya viongozi wa umoja huo.

Alitoa kauli hiyo jana wilayani Kyerwa alipozungumza na Mwandishi wetu.

Mbowe alisema kuwa hawamwamini tena Zitto kwa madai kuwa akiingia Ukawa atakuwa akivujisha siri za umoja huo kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hatuwezi kumruhusu Zitto na chama chake kiwe miongoni mwa Ukawa. Tukiruhusu Zitto awepo siri zote zitakuwa zikiwafikia CCM,” alisema Mbowe.

Aprili 15 mwaka huu, Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), kilitangaza kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa lengo la kuleta mapinduzi ya uchumi na kubomoa mfumo unaowanyonya wananchi.

Zitto alisema hivi sasa taifa limekuwa na shauku ya ACT kushirikiana na vyama vingine kama njia ya kufanikisha malengo ya kukitoa CCM madarakani. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips