Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Showing posts with label ACT- Wazalendo. Show all posts
Showing posts with label ACT- Wazalendo. Show all posts

Waliomdharau Zitto Kabwe Sasa Awafunga Midomo

Jembe letu hili litakuwepo tena mjengoni panapo majaliwa huku wabaya wake wengi wakiwa hawajui hatima yao.

Wabunge weng wa Chadema hawajui hatima yao huku wafuata upepo wa Mbowe kina Wenje, Nyerere, Haines Kiwia, n.k wakiwa wameshapigwa chini.
Quote: What we have, what we wish we had - ambitions fulfilled, ambitions disappointed, investments won, investments lost, elections won, elections lost - these things may occupy our attention, but they do not define us. By Mitt Romney 3

Urais Waivuruga ACT-Wazalendo ya Zitto Kabwe.......Waliyemchukulia Fomu ya Urais Akataa, Asema Hajajiandaa Kisaikolojia

Hali ya hewa ndani ya Chama cha ACT- Wazalendo ambacho kinaongozwa na Zitto Kabwe, imechafuka, baada ya Kamati Kuu kumpitisha na kumchukulia fomu ya urais, Prof. Kitila Mkumbo, huku mwenyewe akisita kulipokea jukumu hilo.

Kufuatia hatua hiyo, Prof. Kitila ameandika katika mtandao wa kijamii kuwa hajaandaliwa kisaikolojia kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais na jukumu hilo wapewe viongozi wengine waandamizi.

Tofauti na ilivyozoeleka kwa wagombea kwenda na wafuasi wao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuchukua fomu za kugombea urais, kwa upande wa ACT – Wazalendo, Katibu Mkuu, Samson Mwigamba, jana alikwenda Nec kumchukulia  fomu Prof. Kitila ambaye inadaiwa viongozi wakuu wa chama hicho wamekutana naye kwa mazungumzo ya kumshawishi akubali kupeperusha bendera ya chama hicho kuelekea Ikulu.

Mapema asubuhi jana Prof. Kitila alifika ofisi za chama hicho Kijitonyama na kuondoka na majira ya saa 5:00 asubuhi wafuasi zaidi ya 100 wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali walivamia ofisi hiyo na kumbana Mwigamba kuwaeleza kwanini chama hicho kinachelewa kuweka wazi mchakato wa mgombea wake wa urais.

Habari zinasema kuwa licha ya Prof. Kitila kutokuwapo kwenye kikao cha Kamati Kuu (CC) kilichopitisha uamuzi wa kumtaka apeperushe bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais, lakini ulipitishwa uamuzi wa kwamba abebe jukumu hilo zito.

Wakati Kamati Kuu ikiamua hivyo, hadi jana alasiri hapakuwapo na makubaliano na Prof. Kitila, lakini viongozi wakuu wa chama walikuwa kwenye mazungumzo naye.

Akizungumza na mtandao huu jana, Mwigamba alisema alichukua fomu hiyo saa 4:00 asubuhi, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Kamati Kuu iliyokutana Agosti 15, mwaka huu.

Alisema pamoja na azimio hilo, Kamati Kuu ilipitisha majina ya wagombea ubunge nchi nzima, wagombea udiwani na kupokea ripoti ya wataalamu washauri juu ya ushiriki katika harakati za uchaguzi wa rais.

“Baada ya kupokea taarifa na mapendekezo yao tukajiridhisha kwa mustakabali wa taifa, chama kinahitaji kusimamisha mgombea urais, ndipo nilipoagizwa kwenda kuchukua kwa sababu muda unaenda zianze kujazwa ili Ijumaa ambayo ndiyo siku ya mwisho zirudishwe,” alisema Mwigamba.

Alisema Kamati Kuu imeamua hivyo kwa kuwa Prof. Kitila ni mwadilifu, mzalendo wa kweli, anaweka mbele maslahi ya Taifa na kwamba ana sifa zote za kuliongoza taifa na mgombea mwenza atakuwa ni Mwandishi wa habari mkongwe, Hawra Shamte.

Hata hivyo, Hawra, alipoulizwa kuhusu maamuzi hayo ya Kamati Kuu, alisema hana taarifa zozote na kwamba hadi jana jioni hakuarifiwa chochote.

Alisema wakati mgombea huyo anakutana na viongozi wakuu wa chama hicho, fomu hiyo itaendelea kusambazwa mikoani ili kusaka wadhamini na kwamba walianza kufanya hivyo jana.

“Tofauti yetu na wengine hatutakuwa na ziara kwenye kusaka wadhamini, nimeenda na wanachama wengine watatu kuchukua fomu na sikuwa na msururu wa watu na hivyo hivyo kwenye kusaka wadhamini itakuwa kimya kimya,” alisema Mwigamba.

Alipoulizwa juu ya utayari wa Prof. Kitila kupeperusha bendera hiyo, alisema: “Hatuna wasiwasi, tunaamini atakubali uamuzi wa Kamati Kuu, anajua ni wajibu kubeba jukumu chama kinapomuhitaji.”

Aidha, Mwigamba alisema kama itashindikana kwa Prof. Kitila, ni lazima chama hicho kisimamishe mgombea mwingine katika nafasi hiyo.

Kitila: Sina Maandalizi
Katika kundi la mtandao wa kijamii la chama hicho la Whatsaap, lijulikanalo kama ACT Taasisi Imara, Prof. Kitila aliandika taarifa ya kuwashukuru wanachama na viongozi kwa imani yao kwake, lakini alisema hawezi kubeba jukumu hilo.

“Naomba niwashukuru nyote kwa imani kubwa mliyonayo juu yangu katika kukiwakilisha chama katika nafasi ya urais, naishukuru Kamati Kuu kwa imani yake kwangu hata kufikia hatua ya kupitisha azimio la kuniomba kugombea urais kwa chama chetu. Jana CC (Kamati Kuu) ilituma ujumbe maalum nyumbani kwangu kwa ajili ya kuzungumza na familia na jamaa zangu juu ya ombi hilo,” alisema katika andiko hilo na kuongeza:

“Nimekuwa nikitafakari tangu Alhamisi nilipoombwa rasmi kutafakari uwezekano wa mimi kugombea baada ya juhudi zetu za kutafuta mgombea kushindikana. Nimefanya mawasiliano mapana ndani ya familia, chama, chuoni ninapofanyia kazi, kanisani kwangu na kwa watu na taasisi mbalimbali ninazohusiana nazo.”

Alisema baada ya tafakari na mawasiliano mapana (consultations), ameona hana utayari na maandalizi ya maana ya kisaikolojia, kifamilia na kisiasa kumuwezesha kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.

“Najua nimewaangusha sana katika uamuzi wangu huu, lakini naamini kwamba mtaheshimu uamuzi wangu na kwamba hamtaacha kuthamini mchango wangu katika chama kwa sababu ya kukataa kugombea urais,” alisema na kuongeza:

“Nasikitika kwa tuhuma ambazo baadhi ya wanachama wetu wanarusha katika mitandao ya kijamii na sehemu nyingine. Nathamini na kuheshimu haki ya wanachama kuonyesha hasira kwa jambo wasilolipenda…nawasihi wanachama wajizuie kuzusha mambo yatakayochochea chuki ndani ya chama na kukatishana tamaa.”

Aidha, alishauri wanachama wengine waandamizi waombwe wachukue jukumu hilo na kuwataja kuwa ni Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo na Katibu Mkuu, Mwigamba na kwamba wakati hayo yakitafakariwa wasisahau malengo mapana ya chama waliyojiwekea katika uchaguzi huo.

Alisema mafanikio waliyofikia ni kuweka wagombea ubunge na udiwani kata na majimbo mengi nchini.

Mwigamba alipoulizwa juu ya taarifa hiyo, alijibu: “Sina simu ya whatsaap ila naenda kwenye kikao hadi leo (kesho) nitawapa taarifa.”

Wafuasi wakusanyika
Baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wanachama na wafuasi wa ACT-Wazalendo yalikuwa na ujumbe wa ‘wamenunuliwa’ na mgombea wa Chadema, Edward Lowassa ili wasisimamishe mgombea urais.

Wafuasi hao walikaa kwa saa nne nje ya ofisi hizo wakiimba nyimbo mbalimbali.

Mabango mengine yalisomeka: “Viongozi hatuwaelewi mmekaa muda mrefu bila kutuambia mgombea urais ni nani wakati muda unaisha, kama hamsimamishi mgombea ni bora mfunge ofisi, tusijihusishe tena na siasa, liko wapi azimio la Tabora?”
3

Ukimya Wa Zitto Kabwe Na ACT yake Kunani?

Simsikii tena zzk na zile harakati zake za kuitangaza ACT kulikoni?
Au ndio "safari ya kukata tamaa imeanza"? 
Au ndio kusema kimya kingi kina mshindo?
Rudi Bwana Zitto Kabwe tuna kuhitaji sana katika tasnia hii ya siasa za kibongo!

Tanzania Hottest Celebrity Gossip News 3

Atimae Zitto Kabwe Achukua Form ya Kugombea Ubunge..Unataka Kujua Atagombea Wapi ? Soma Hapa

Safari ya mbunge wa zamani wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe kurejea bungeni imeanza rasmi baada ya kiongozi huyo wa chama kipya cha ACT-Wazalendo kuchukua fomu za kuwania kuongoza jimbo la Kigoma Mjini.

Uamuzi huo wa kulitaka jimbo hilo unathibitisha kauli zake ambazo amekuwa akizitoa kwa muda mrefu kuwa hatarudi tena Kigoma Kaskazini kwa kuwa alishawatimizia kila kitu na haoni sababu za kuwawakilisha tena wananchi wa eneo hilo.

Kauli yake iliibua ubashiri kuwa Zitto anataka kubadilishana jimbo na mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, uvumi ambao aliukanusha akisema hadhani kama CCM inaweza kupata jimbo Kigoma.

Zitto, ambaye alijiondoa Chadema baada ya kukiuka katiba kwa kufungua mashtaka dhidi ya chama hicho, hakufanya mbwembwe wakati akienda kuchukua fomu kwenye ofisi za ACT Ujiji jana, badala yake aliita viongozi wa kata na matawi bila ya kutaarifu vyombo vya habari.

Nimeamua kugombea ubunge wa Kigoma Mjini ili niwatumikie ndugu zangu ambao wamekuwa wakipata tabu katika kupigania haki zao za msingi ambazo walistahili kuzipata kama ilivyo katika mikoa mingine,” alisema Zitto alipoongea na mwandishi wa Mwananchi kwa simu.

Nitakapokuwa mbunge wa Kigoma Mjini nitahakikisha barabara za mitaani zinapitika katika kipindi chote cha mwaka, nitahakikisha watu wanaacha tabia ya kulima mashamba katikati ya mitaa na makazi, lakini nitahakikisha kila mmoja anajiunga na mifuko ya kijamii ili kujiwekea akiba ya uzeeni pamoja na kupata huduma ya matibabu, elimu na nyinginezo zinazopatikana kwa kutumia mifuko hiyo.”

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema bonde la Mto Luiche bado halijatumika ipasavyo kuzalisha chakula kwa wingi.

Nakusudia kuibana Serikali ijenge skimu ya umwagiliaji maji ili wakulima walime kilimo cha mpunga kwa mwaka mzima bila kupumzika, jambo ambalo litainua uchumi wa wakulima na kuongeza chakula hapa Kigoma,” alisema.

Kuhusu umeme wa gridi ya Taifa, Zitto alisema lazima upatikane ili kusaidia jitihada ya ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi na kilimo kwa kuwa hivi sasa mji wa Kigoma Ujiji unategemea umeme wa jenereta ambao hauwezi kuendesha shughuli za viwanda, hali inayochangia mkoa kuendelea kuwa masikini licha ya kuzungukwa na rasilimali nyingi.

Katibu wa ACT wa Jimbo la Kigoma Mjini, Azizi Ally alisema Zitto alichukua fomu hiyo jana kwa malipo ya Sh100,000 mbele ya viongozi 72 wa kata na matawi kutoka jimboni humo.

“Kwa hali ya sasa Kigoma Mjini inahitaji kupata mbunge anayeweza kufuatilia mambo kwa kina ili kuleta maendeleo ya wananchi baadala ya yule anayekwenda bungeni kujifunza,” alisema Ally.

Watu wanakabiliwa na kero mbalimbali kama ubovu wa barabara za mitaani, uhaba wa umeme wa uhakika unaoweza kuendesha viwanda vikubwa na vidogo, pamoja na wengi kufanya kilimo cha kujikimu zaidi.“

Zitto alitofautiana na uongozi wa juu wa Chadema uliomtuhumu kuwa alikuwa amefanya uasi na kwamba alishaanzisha chama kingine akiwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani na kusababisha avuliwe nyadhifa zote, ikiwamo ya unaibu katibu mkuu.

Hata hivyo, wakati Chadema ikijiandaa kumjadili na pengine kumvua uanachama, Zitto alifungua kesi akitaka mahakama imuamuru katibu mkuu wa Chadema ampe nyaraka za mwenendo wa vikao vilivyomvua madaraka na kuomba amri ya kuzuia vikao hivyo visimjadili.

Katika hukumu ya kesi hiyo, mahakama ilitupilia mbali hoja zake, uamuzi uliotafsiriwa kuwa umefungua njia ya kutimuliwa kwake kwa kitendo cha kufungua kesi mahakamani kinyume cha katiba.

Mkazi wa Gungu mjini Kigoma, Zuberi Mrisho alisema ujio za Zitto kugombea Ubunge wa jimbo hilo utaamsha ari ya wananchi kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Wapigakura na kujitokeza kupiga kura tofauti na chaguzi zilizopita.

Mwaka 2010 Vijana wengi hatukupiga kura hapa kwa sababu tulikosa imani na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali, lakini kwa ujio wa Zitto sasa nina hakika wengi tutajitokeza kupiga kura ili tupate viongozi makini kwa maslahi ya mji wetu,’ alisema Mrisho.
3

Zitto Kabwe awanyima usingizi CHADEMA, viongozi wahaha nchi nzima kuzima moto wa ACT

Wadau, hakika sasa si siri tena kwamba kitendo cha uongozi wa CHADEMA kumfukuza uanachama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kumekigharimu chama.

Mtakumbuka kuwa baada tu ya Tundu Lissu kutangaza kuwa Zitto Kabwe si mwanachama tena wa chadema baada ya Mahakama kufuta kesi aliyoifungua dhidi ya uongozi wake, Zitto Kabwe alitangaza kuachia madaraka ya ubunge na hatimaye kujiunga na ACT ambapo amechaguliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa chama hicho.

Kitendo hicho cha Zitto kuhamia ACT kilipokelewa kwa dhihaka na makada wa CHADEMA wakidhani kuwa Zitto Kabwe ndo anajimaliza kisiasa. Hata hivyo, baada ya Zitto Kabwe kuhamia ACT na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama hicho, alifanya ziara katika mikoa 10 nchini akiwa na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu Samson Mwigamba. Umati uliofurika kuhudhuria mikutano ya ZITTO umewashtua sana viongozi wa CHADEMA. Kilichowashtua zaidi ni maelfu ya wafuasi wa chadema walioacha chama hicho na kujiunga na ACT.

Hakika Zitto Kabwe amechafua hali ya hewa ya Kinondoni Mtaa wa Ufipa. Sasa viongozi wanaona viti vinawaka moto. Sasa wanaona kuwa chadema inaelekea kwa Buriani. Ni kutokana na amsha amsha ya Zitto Kabwe na mchaka mchaka aliouanza, Viongozi wa CHADEMA hawana namna nyingine zaidi ya kukabiliana naye kwenye majukwaa na njia za siri.

Kwa upande wa majukwaani, Kamati Kuu ya chama hicho imeagiza kuwa viongozi wote wasambae mikoani kuzima moto wa Zitto Kabwe. Haijapata kutokea viongozi wakuu wote wakaikimbia ofisi ya CHADEMA kama ilivyo sasa. Kuanzia Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Manaibu Katibu wakuu wote wanapita maeneo aliyolisha sumu Zitto Kabwe ili kujaribu kutoa maziwa ambayo wanaamini pengine yanaweza kukata sumu hiyo. Lakini wapi.

CHADEMA sasa wanalia na kusaga meno. CHADEMA wanajutia maamuzi waliyofanya. Wataalam wa masuala ya siasa wanaona kuwa nguvu ya Zitto Kabwe katika kushawishi inazidi mara dufu uwezo wa viongozi wote wa UKAWA. Washauri wa CHADEMA akiwemo Saed Kubenea wanaona kuwa Zitto Kabwe akiachwa aendelee atasababisha nguvu ya UKAWA kumezwa na ACT.

Kwamba ACT itageuka kuwa chama kikuu ya Upinzani baada ya uchaguzi wa Oktoba 2015 ambao bila shaka CCM itashinda kwa kishindo. Aidha, jaribio la kumshawishi Zitto Kabwe kujiunga na UKAWA zinaelekea kugonga mwamba hasa baada ya John Mnyika kujichanganya alipotangaza kuwa Zitto Kabwe ni adui namba moja wa CHADEMA.

Imeandikwa na  Lizaboni/JF3

MBOWE Apigilia Msumari Kauli Ya Mnyika.....Asema Hawatamruhusu Kiongozi wa ACT Zitto KABWE Kujiunga na UKAWA kwa Madai Kuwa Atavujisha SIRI Zao

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema hawatamruhusu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Kauli ya Mbowe imetolewa siku chache baada ya Zitto kutangaza kuwa ACT ipo tayari kujiunga na Ukawa kama wanavyotaka Watanzania wakiwamo baadhi ya viongozi wa umoja huo.

Alitoa kauli hiyo jana wilayani Kyerwa alipozungumza na Mwandishi wetu.

Mbowe alisema kuwa hawamwamini tena Zitto kwa madai kuwa akiingia Ukawa atakuwa akivujisha siri za umoja huo kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hatuwezi kumruhusu Zitto na chama chake kiwe miongoni mwa Ukawa. Tukiruhusu Zitto awepo siri zote zitakuwa zikiwafikia CCM,” alisema Mbowe.

Aprili 15 mwaka huu, Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), kilitangaza kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa lengo la kuleta mapinduzi ya uchumi na kubomoa mfumo unaowanyonya wananchi.

Zitto alisema hivi sasa taifa limekuwa na shauku ya ACT kushirikiana na vyama vingine kama njia ya kufanikisha malengo ya kukitoa CCM madarakani. 3

ACT-Tanzania Wabadilisha Rasmi Jina la Chama

Chama kipya cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kimebadili jina lake la awali la ACT-Tanzania.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini imekubali maombi ya chama hicho huku ikiwataka kurudisha cheti cha usajili wa awali na kupewa cheti kingine.

Awali ACTL-Wazalendo ilipata usajili kwa jina la ACT-Tanzania na baadae kuomba kulibadili jina hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, ameridhika na maelezo yaliyokuwa yametolewa na uongozi wa chama hicho wa sababu za kuamua kubadili jina la chama hicho kutoka ACT-Tanzania hadi ACT-Wazalendo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari jana jiijini Dar es Salaam, Jaji Mutungu alijibu ombi hilo kwa njia ya barua.

Katika taarifa hiyo inaeleza: "Nikurejeshe kwenye barua yenye kumbukumbua namba AC-HQ/MSJ/2015 ya Aprili 15, mwaka 2015 ikisomwa sambamba na barua yangu yenye kumbukumbu namba HA.322/362/20/80 ya Aprili 13, mwaka 2015 kuhusu suala tajwa hapo juu".

Jaji Mutungi alieleza kuwa, alisoma na kuyatafakari kwa kina maelezo katika barua ya ACT-Wazalendo, na kwamba ameridhika na maelezo yao kuhusu jina jipya la chama hicho kwa mujibu wa kanuni ya 7 ya kanuni za usajili wa vyama vya siasa.

Chanzo: Nipashe 3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips